NGUVU NA MAFANIKIO ❤‍🔥


Kila mwanadamu anahitaji NGUVU ili kufanikiwa sana katika maswala mbalimbali. Wapo watu wanao tumia nguvu za giza na wapo watu wanatumia NGUVU za Mungu. Mifano mbalimbali kwenye biblia;

Ayubu
▪️Ayubu 42:10
Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.

Ayubu alikuwa tajiri na anapata kufanikiwa kwasababu alikuwa na NGUVU nyuma yake zinazo msaidia kufanikiwa. Ukiwa huna NGUVU za rohoni huwezi kutawala katika eneo flani.

Daudi
▪️1 Samweli 16:13
[13]Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya BWANA ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

Tangu hapo Daudi akawa na uwezo wa kipekee hata kupata kibali kwa mfalme na kila alilolifanya lilifanikiwa.

Eliya
▪️1 Wafalme 18:46
[46]Mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya; akajikaza viuno, akapiga mbio mbele ya Ahabu mpaka kuiingia Yezreeli.

Mkono wa Bwana ulipomshukia Eliya akapata uwezo wa kwenda kwa kasi zaidi ya magari ya farasi.

Kipofu kuzaliwa
▪️Yohana 9:1-3,7
[1]Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.
[2]Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
[3]Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
[7]akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.

Nguvu zilifanyika thabiti kwasababu tu Mungu ajitwalie utukufu.

Je ni namna gani ya kupata hizi NGUVU?
▪️Mathayo 5:6
Heri wenye njaa na kiu ya haki;
Maana hao watashibishwa.

1)Uwe na nia ya kumshuhudia YESU kupitia hicho unachoombea NGUVU kwacho.

▪️Yakobo 4:3
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

▪️Matendo ya Mitume 1:8
[8] Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Swali je Bwana aweza kukuamini na NGUVU zake? NIA YA NDANI ndio funguo ya Bwana kukuamini na NGUVU zake mbali na hapo utafanya kama ilivyo kawaida ya mtu asie na nguvu.

Nabii Nuru 💡

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started