(Series)
BY. MARIA FESTO
Kwanza kabisa Mungu ni pendo .Na pendo lake kwetu linathibitishwa na sadaka ya mwanae Yesu Kristo
Hivyo utoaji unaambatana na upendo
Neno utoaji linamaanisha kumpa mtu kitu au vitu
Tukisoma Yohana 3:16
Mungu anaonyesha jinsi alivyofanyika kielelezo halisi Cha utoaji
Naomba tusome wote kwa pamoja
John 3:16
[16] Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Maandiko yanathibitisha jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu mpaka akadiriki kumtoa mwanae wa pekee
Kwahiyo utoaji wowote lazima uzingatie Mambo makuu matatu
1.Upendo
2.Nia njema
3.Utakatifu
Utoaji wako unaonyesha vile unavyompenda,unavyomtii na kumwamini Mungu.
Utoaji unampa Mungu nafasi ya kujua ni kiwango gani unamuheshimu na kuthamini Mambo anayofanya kwenye mais ha yako
Kiukweli neno utoaji kibibilia ni Jambo pana Sana.
Utoaji unaweza ukawa ibada unayomfanyia Mungu,muda unampa Mungu, au sadaka unazompa Mungu kwa moyo Safi ,upendo na nia njema
Utoaji ni mapatano kati ya mtu na Mungu. Ndiyo maan unaweza kumjaribu Mungu kupitia kutoa na Mungu anaweza kuutazama Moyo kupitia kutoa kwako
Ngoja tuendelee mbele kidogo tuone vyanzo vya utoaji.
“`~Vyanzo vya utoaji““
Vyanzo vya utoaji viko vingi Sana Kama
1.biashara
2.kazi
3.kilimo
4.ufugaji
5.Kipato chochote Cha halali
Kupitia hivi vitu unaweza kumtolea Mungu sadaka.
Mfano mfugaji unaweza kutoa mifugo au ukauza mifugo yako na ukatoa fedha,mkulima unaweza toa mazao mazuri,mfanya biashara na mfanyakazi Hali kadhalika pia unaweza kumtolea Mungu sehemu ya mshahara au kipato chako
NB: Mungu hapaswi kupelekewa matolea au sadaka dhaifu.Na hatutoi kwasababu Mungu ana shida na matoleo yetu.Bali sababu tunampenda na kumuheshimu Mungu
Mungu ni utoshelevu
Embu tuangalie sasa
kwanini tunatoa?
Tunatoa ili kupata thawabu kutoka kwa Mungu
Embu tuangalie injili ya mathayo 6:1
Matthew 6:1
[1] Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
You see the reason of giving is to get rewards from God and not man.
Ndiyo maana anasema angalia msifanye wema machoni pa watu.
2.Tunatoa kwasababu tunampenda Mungu
Bibilia iko wazi kabisa ikionyesha kwamba Bwana Yesu amekua kielelezo namba moja katika utoaji
Ndiyo maana alikubali kuacha enzi na vyote na kuutoa uhai wake ili tuokolewe
You see the Love of Jesus is very powerful than death
Rejea Yohana 3:16
You see the way you give represent your love toward God
3.kutoa kunaonyesha utii wetu kwa Mungu
You see ilimgharimu Bwana Yesu kutoa uhai wake kwasababu ya utii wake kwa Mungu
The way you give show how humble you are before God
Kwasasa naomba niishie hapo nikipata neema Tena tutakuja kuangalia vipengele vifatavyo
1.kanuni za utoaji
2.Aina za watoaji
3.Aina za matoleo
4.Faida za kutoa
Itaendelea….
© HEAVENLIFE NETWORK MINISTRIES
